NCHI IPO PABAYA SANA.
N chi yetu ya Kenya ipo pabaya Sana . Inahitaji Dua eti! Wanadani watu eti kuishi nchi hii tukufu ya Kenya ni kurithi mateso na bughdha. Hivi Sasa mbele hakuendeki na nyuma hakurudiki! Maisha ya Sasa Nchini Ni Bora usalama tu . Kupata rizki Ni bahati na miujiza . Ukipata chajio sahau staftahi na ukipata staftahi sahau chajio. Yani kila kukicha afadhali ya Jana. Uchumi wa nchi hii umesambaratika pakubwa. Kwa Sasa wananchi kuyamudu mahitaji yao Ni changamoto. Mafuta ya kupikia yanauzwa Bei sawa na magari ya kifahari! Chai Ni ya mkandaa tu. Bei ya maziwa Ni sawia Ni sawia na kununua ardhi. Yote haya yanajiri huku kukiwa na baa la njaa na pia athari za Corona zingalipo. Je, tumlaumu Nani kwa Visa hivi vyote? Wananchi wao ndo wanafaa kujilaumu kwa kuwa viongozi wanaowachagua wao ndo wanafaidi wenye kwa kupora Mali na fedha ya wananchi. Sasa imefika wakati wananchi wa kenya kuamka na kutoka kwa lepe ya usingizi ya kuchagua viongozi wasiofaa. Shukran kwa kupitia m...